Vipeperushi Vya Injili

Vipeperushi Vya Injili
(Gospel Tracts) Vilivyoandikwa
Na Askofu Rodrick Mbwambo

Kanisa la Maranatha Reconciliation linaamini katika Utume Mkuu aliotuachia Bwana Yesu wa kuifikisha Injili Tanzania na duniani kote kwa ujumla. Kama umeandaa kampeni ya ushuhudiaji unaweza kuagiza idadi yoyote ya vipeperushi unayohitaji.
Gharama za kuchapa na matayarisho utalipia, pamoja na usafirishaji. Mathayo 28:19–20

NI ZAIDI YA VIRUSI

Kipeperushi hiki kina ujumbe maalum wa Injili kwa ajili ya watu ambao safari yao ya kimaisha inaonekana kufikia tamati kutokana na ukweli kwamba wako katika hali ya umauti na hawana mahali pa kutokeo; isipokuwa kulingojea kaburi. Lakini pamoja na sitofahamu hiyo, ndani ya kipeperushi cha Zaidi ya Virusi utakutana na matumaini na ushindi mkubwa kupitia jina kuu la Yesu Kristo.

© 1997 Askofu Rodrick Mbwambo.
All rights reserved.

Go and make disciples of all nations.

SIMU YENYE UTATA

Simu Yenye Utata (Zamani kilikuwa kinajulikana kama “Simu Kutoka Kuzimu), kina hazima njema ya kumtoa mwenye dhambi kutoka kwenye giza lililokamata moyo wake, kwa kumfunilia madhara anayoweza kuyapata endapo hatamkubali Yesu. Kinaufunua ukweli wote kama ulivyoandikwa kwenye Biblia Takatatifu unaowaagiza wanadamu wote watubu dhambi zao ili waweze kuokolewa na kupokea Uzima wa Milele.

© 1997 Askofu Rodrick Mbwambo.
All rights reserved.